Jumanne, 18 Machi 2014

Na Mtaalam Siwayombe.

Ile hadithi ya kufikirika iliyoanzishwa na shirikisho la Kandanda hapa nchini [TFF] ya kuanzia safari ya kuelekea fainali za mataifa huru ya Afrika nchini Moroco hapo mwakani inazidikushika kasi baada ya jana Msemaji wa kuajiriwa wa taasisi hiyo kubwa inayosimamia soka la nchi hii kutangaza majina ya vijana 36 ambao watawekwa kambini katika mji wa Tukuyu Mkoani Mbeya kujiandaa na safari ya kuelekea Uholanzi kwa ajili ya mafunzo rasmi ya miezi mitatu kabla ya kuanza kampeni ya kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali za Moroco hapo mwakani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Bonifac Wambura ni kuwa umri wa vijana hao ni miaka 21 hivyo kutoa nafasi ya kudumnu katika kikosi hicho kwa muda mrefu kama viwango vyao havitatetereka.
Bado maswali yanazidi kuwa mengi kwa wadau wa soka hapa nchi juu ya mpango huo kufanikiwa kutokana na aina ya mfumo uliotumika kuwapata vijana hao kutokana na kutojulikana chimbuko la vijana hao katika soka limetokea wapi hivyo kuzua hiofu juu ya muda mfupi wa kambi kama utatoa majibu sahihi ya kilichokusudiwa.
Kila mwanamichezo hususani mchezo wa mpira wa miguu ana wajibu wa kutafakari hilo kwa makini kutokana na misingi ya soka kuwa wazi na njia zake za mafanikio kujulikana na hivyo kila mmoja ajiulize kama nchi tumezingatia njia hizo kwa usahihi ili kufikia mafanikio tunayoyahitaji?
Sote kwa pamoja tukae tusubiri wataalam walioamua kutupitisha katika njia hiyo ya mkato kama itatoa matunda yanayotarajiwa.
kwa leo ni hayo tu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni